TAHARUKI YAZIDI KWENYE SEKTA YA UCHUKUZI KISIWANI MOMBASA
Ni takriban siku tatu tangu waziri wa uchukuzi kaunti ya Mombasa Taufiq Balala pamoja na kamati husika kubadilisha mfumo wa magari kuingia na kutoka kwenye kisiwa cha Mombasa huku wakifunga baadhi ya barabara na mizunguko ili kupunguza tatizo la msongamano wa magari katika kaunti hio
Tarehe 2 mwezi wa 2 mwaka wa 2022 ndio ukurasa mpya uliobadilisha mfumo wa magari kaunti ya Mombasa huku njia zilizotumika tangu enzi za mkoloni zikibadilishwa na kustaajabisha wengi
Magari makubwa yamezuliwa kuingia kisiwani kutoka saa moja asubuhi hadi saa moja jioni huku adhabu kali ikiwekwa kwa watakaokiuka sheria hio
Akiongea kwenye steji ya sabasaba waziri huyo amekiri kwamba ni wakati wa kuamua mabadiliko yatakaopunguza msongamano huku akisistiza kwamba changamoto zipo na itachukua muda kwa wakazi wa Mombasa kuzoea mfumo hio
Aidha kwa upande wa wachukuzi kaunti ya Mombasa ikiwemo, bodaboda, madereva wa tuktuk na marathon wameghadhabishwa na mfumo huo huku wakidai kwamba hawakuhusishwa kivyovyote wala idara husika hazikuwepo kwenye vikao vya kubadilisha mfumo huo
Shirika husika katika maswala ya barabara ni KENHA limejitoa mbali huku wakidai mfumo huo ni ukiukaji wa sheria na hawakuhusishwa kivyovyote
Takriban watu kumi na sita wanauguza majeraha katika hospitali kuu kaunti ya Mombasa huku wawili wakipoteza maisha kwenye ajali ya barabara ni tangu mfumo huo uanze
Abiria wamelalamika baada ya nauli kupandishwa maradufu huku wakidai kwamba hali imezidi kuwa tete kwao Ali Omar mkazi wa Bamburi amesema kwamba hivi sasa anatumia karibu Mia tatu kwenye nauli ukilinganisha na shillingi mia moja hapo awali
Aidha madereva wa matatu na tuktuk wamesema kwamba mizunguko imekuwa mingi ikiwapelekea kuongezeka kwa matumizi ya mafuta huku abiria wakikosekana kwenye stendi za matatu.
Shwari
ReplyDeleteKazi kuntu
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi safii kaka
ReplyDeleteKAZI kuntu Sana .Heko!
ReplyDeleteHeko !
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteViongozi mwatudhalilidha watu wamombasa na kutuzidishia Kua maskini
ReplyDeleteKisha mm binafsi Hua najiuliza hawa viongozi walipatajepataje vyeo kama hivyo na ilhali Hawajui chochote
Bwana Taufiq nakwambia ukitaka kubadilisha mfumo wakuendesha magari barabarani kwanza panua Barabara uitengeneze ipaswavyo kisha uwajulishe wakaazi wa maeneo hayo ndipo mutaenda msururu ulio nyoka
Viongozi wacheni siasa mbovo
Tushawajuaaaaa
Wana Mombasa HATUPANGINGWI
Swadakta
ReplyDelete❤
ReplyDeleteππΎππΎ
ReplyDeleteYaudhi sana Wananchi kuachwa nje wakati wa maamuzi yanayowahusu
ReplyDeleteKazi nzuriii
ReplyDeleteπ₯π₯π₯
ReplyDeleteNice one
ReplyDeleteInsight
ReplyDeleteSahii maisha magumu kweli
ReplyDelete